Mafanikio ya Wanawake Tanzania Yamshangaza Makamu Rais wa Hispania

Mama Maria Tereza akisisitiza jambo wakati akitoa shukrani zake kwa wanawake wa Tanzania wanaofanya miradi mbalimbali ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.   MAKAMU wa Rais mstaafu wa Hispania, Maria Tereza Fernandes de la Vega Sanz (67), amesema kwamba amefurahishwa mno na mafanikio ya wanawake 15 wa Tanzania katika kipindi kifupi baada ya mafunzo waliyoyapata jijini Madrid mapema mwaka huu. …