Na Mwandishi wetu BODI ya manunuzi na ugavi (PSPTB) imetoa mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya manunuzi na ugavi katika chuo cha uhasibu(TIA) Mbeya. Katika mafunzo hayo wito ulitolewa kwa Taasisi binafsi na serikali kuepuka kutoa ajira katika sekta ya manunuzi na ugavi kwa watu ambao hawana taaluma hiyo wala kusajiliwa na Bodi ya PSPTB. Wito huo ulitolewa na Mwakilishi …
Wanafunzi Waonywa Kuhusu Maambukizi ya VVU
Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi WANAFUNZI wametakiwa kujiepusha na vitendo vitakavyochochea wao kupata maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na mimba za utotoni jambo litakalowafanya wakatize masomo na hivyo kutotimiza ndoto za maisha yao. Rai hiyo imetolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati …
Wazazi Kutubagua Watoto wa Kike Kielimu ni Ukatili – Wanafunzi
BAADHI ya wanafunzi wa kike katika Shule ya Msingi Nachitulo Wilayani Newala wamewataka wazazi kuacha tabia ya kuwabagua watoto wa kike kielimu kwani kufanya hivyo ni kumnyanyasa mtoto wa kike kijinsia. Wanafunzi hao walitoa kilio hicho hivi karibuni katika mjadala uliofanyika kwenye shule hiyo uliokuwa ukijadili vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na uelewa wa vitendo hivyo kwa watoto ili kuweza …
TPB Yawapa Somo la Akiba Wanafunzi Sekondari ya Jangwani
WAZAZI na walenzi wametakiwa kuwa na mazoea ya kuwawekea watoto wao akiba ili iweze kuwasaidia katika mambo mbalimbali ikiwemo elimu. Mwito huo umetolewa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Nchini (TPB) Sabasaba Moshingi, wakati wa semina iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Jangwani. Alisema, katika kuadhimisha miaka 90 ya siku …
Wanafunzi wa Awali Tunduru Wasomea Chini ya Mti
Na Joachim Mushi, Tunduru WANAFUNZI wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Nakayaya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wanasomea chini ya mti kutokana na darasa hilo kuendeshwa bila ya kuwa na chumba maalum kwa ajili ya kusomea wanafunzi hao. Hali hiyo imebainika baada ya mwandishi wa habari hizi kuitembelea shule hiyo hivi karibuni na kuwakuta wanafunzi wakiwa wamekaa chini …
Wanafunzi Msingi Wampa Ujumbe wa Rushwa Rais Kikwete
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Fatma S. Ally alipowasili wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi Rais Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali wilayani humo Rais Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali wilayani humo Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Mtera Mhe Livingstone Lusinde “Kibajaji” Kikundi cha utamaduni cha Shule ya …