Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM, Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, leo wamefunga Ofisi ya Taasisi ya Mikopo ya WADOKI (Wadoki Saccos) pamoja na Hotel ya KIRUMBA RESORT kutokana na watajwa kushindwa kulipia kodi ya pango. Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kirumba Acheni Maulid (anaeongea pichani) amesema kuwa wanachama hao wamefikia maamuzi hayo kutokana na kutumia majengo …