Wamiliki wa Blogu Tanzania Wateua Kamati ya Muda Kuongoza…!

WAMILIKI wa Mitandao ya Kijamii Tanzania wameteua viongozi wa muda ambao watafanya kazi ya kushughulikia usajili wa Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya kijamii (Bloggers) ili kuwaunganisha waendeshaji wa mitandao hiyo ya kijamii Tanzania. Uteuzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mlimani City kwenye mkutano wa mafunzo ulioandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) …