MKUU wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu ameitaka Halmashauri ya Jiji hilo kutenga maeneo maulumu ya kuwawezesha wafanyabiashara wenye ulemavu kufanya shughuli za kujiingizia kipato badala ya kuwatumia mgambo wa jiji kuwabughudhi. Nkurlu ametoa kauli hiyo kwenye mkutano na watu wenye ulemavu uliofanyika kwa lengo la kutambua changamoto zinazowakabili na namna ya kuzipatia ufumbuzi na kuwakabidhi kadi ya Bima ya …
Rais Dk Pombe Magufuli Awakuna Walemavu, Wampongeza
Na Skolastika Tweneshe na Nyakongo Manyama, Maelezo SHIRIKISHO la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph kwa kumteua Dk. Abdallah Possy kuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na Walemavu). Dk. Possy ambaye pia ni ambaye ni Mwalimu katika Chuo Kikuu cha …
CHAVITA Yasikitikia Ushiriki Mdogo wa Viziwi Uchaguzi Mkuu
Na Zawadi Msalla CHAMA Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kimesikitishwa na kitendo cha ushiriki mbovu wa Viziwi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba kote nchini. Akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Habari-MAELEZO leo, Mshauri Mwelekezi wa Elimu ya Uraia kwa Watu wenye Ulemavu, Bw. Novat Rukwago alisema kuwa, licha ya jitihada mbalimbali ambazo walijaribu kuzifanya ili kuhakikisha …
StarTimes Yasaidia Watoto Shule ya Walemavu wa Akili Airwing
Kutoka kulia ni wafanyakazi wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi. Elena Liu na Paulina Kaka wakifurahia jambo pamoja na Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Airwing, Kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili, Bw. Issa Mkasa wakati wa kukabidhi msaada wa vyakula na mahitaji mengineyo shuleni hapo. Akishuhudia tukio hilo kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Bi. Fabiola Malisa. …
Walemavu Wafunga Barabara ya Kawawa Dar, Shughuli Zasimama
WAFANYABIASHARA ndogondogo wenye ulemavu eneo la Mchikichini, Karume jijini Dar es Salaam wamefunga barabara kwa zaidi ya saa nne wakishinikiza kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ili wafikishe kilio chao cha kuvunjiwa maeneo yao ya Biashara pamoja na kuibiwa mali zao wakati wa zoezi la vunjavunja mabanda na meza zao za biashara. Zoezi la uvunjaji limefanyika usiku …
Kituo cha Walemavu cha Buhangija Chaomba Zahanati…!
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga MKUU wa Wilaya ya Shinyanga Anne Rose Nyamubi ameomba jamii ya Watanzania kusaidia kupatikana kwa Zahanati katika Kituo cha kulelea watoto walemavu cha Buhangija ili kupunguza adha wanazopata watoto hao katika huduma za afya. Kauli hiyo ameitoa katika mazungumzo na mwandishi wa habari hizi ambaye alifika katika kituo hicho akiambatana na ujumbe wa Umoja wa Mataifa …