Mtafiti Kiongozi Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Nicholaus Nyange (katikati), akizungumza na wakulima wa Wilaya ya Rorya Mkoani Mara katika mafunzo ya siku moja kwa wakulima hao ya kutumia simu kupashana habari za kilimo na kujua changamoto zinazo wakabili. Kulia ni Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia za Kilimo Afrika (OFAB), Daniel Otunge na kushoto ni Mtafiti …
Agrics Yakabidhi Mbegu za Mahindi na Alizeti kwa Wakulima Mikoa ya Shinyanga na Simiyu
KAMPUNI ya Agrics imetimiza ahadi ya kuwakabidhi mbegu bora za mahindi, alizeti na mbolea wakulima wa Maswa, Meatu na Shinyanga vijijini. Zoezi hili limefanyika kwa wakati kufuatia msimu mpya wa kilimo kutazamiwa kuanza hivikaribuni. Kampuni ya Agrics iliwapa fursa wakulima kuchagua aina ya mbegu wazitakazo ili kuhakikisha wanapata kile wakipendacho.Wakulima wanaendelea kuandaa mashamba yao huku wakiwa huru kabisa kwani tayari …
BRN Yapongezwa kwa Kuwasaidia Wakulima Wadogo
Na Mwandishi Wetu MPANGO wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) umepongezwa kwa kuweka katika moja ya sekta zake za kipaumbele, miradi ya kilimo inayolenga kuwasaidia wakulima wadogo nchini. Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam jana na Mwakilishi wa Rais wa Mpango wa UN wa Kusaidia Uwekezaji katika Kilimo (IFAD), Yaya Olanirani, wakati ujumbe wa taasisi hiyo ulipokutana na watendaji mbalimbali …
Bilioni 111 Zatumika Kununua Mazao kwa Wakulima.
SERIKALI imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima katika kipindi cha mwaka 2013/2014 ikiwa ni malipo kwa wakulima baada ya kuiuzia nafaka Serikali. Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Charles Walwa wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akieleza mafanikio yaliyofikiwa …