SERIKALI ya Tanzania imewataka wakimbizi wote ambao walikuwa wanajeshi kutoka nchi walizokuwepo, kuripoti kwenye mamlaka husika ili waweze kupewa uangalizi maalum (special protection) kama wanajeshi. Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (Mstaafu) Emmanuel Maganga, wakati wa maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani yaliyofanyika kambi ya wakimbizi Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Alisisitiza kuwa …
Wakimbizi 126,000 wa Burundi Wakimbilia Tanzania, UN Yasaidia…!
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametoa dola za Marekani milioni 100 (US$ 100m, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 220) kutoka katika Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF) kwa shughuli za misaada katika maeneo tisa yenye dharura duniani na yasiyo na fedha za kutosha. Tanzania—ambayo kihistoria imepokea mamilioni ya wakimbizi kutoka nchi jirani …
Waziri Mkuu Majaliwa Ateta na Wakimbizi, Azungumzia Ngono Zembe
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewaasa raia wanaokimbia nchi zao na kupata hifadhi Tanzania kutobeba silaha wanapoingia nchini kuja kuishi kwenye kambi za wakimbizi. Ametoa onyo hilo Desemba 29, 2015 na wakati akizungumza na mamia ya wakimbizi wanaoishi kwenye kambi za Nyarugusu na Nduta zilizoko wilayani Kasulu na Kibondo, mkoani Kigoma waliofika kumsikiliza kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika kwenye kambi hizo. …
UNHCR: Tanzania ni Kimbilio Salama la Wakimbizi…!
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi Duniani (UNHCR) limesema kuwa Tanzania imekuwa kimbilio salama la wakimbizi kwa sababu ni nchi salama, ni nchi tulivu, ni nchi yenye mahusiano mazuri ya kijamii na yenye kuongozwa na sera nzuri na za kibinadamu. Aidha, shirika hilo, limeiomba Tanzania kutoa ardhi ya kutosha ili kuliwezesha shirika hilo kujenga miundombinu na huduma kwa ajili …
Wakimbizi wa Burundi ‘Wang’ang’ania’ Kurudi Tanzania…!
Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, Sospeter Christopher Boyo (aliyesimama mwenye shati la kitenge) akisoma taarifa fupi ya Kambi ya Nyarugusu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (aliyeketi mwenye suti ya kijivu) aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja …
UNDP, Waziri Chikawe Watembelea Kambi ya Muda ya Wakimbizi Kigoma
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) akiongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa tatu kushot0) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (katikati), Mwakilishi wa Shirika la Umoja …
- Page 1 of 2
- 1
- 2