Wakenya Zaidi 20 Wauwawa Mkoa wa Pwani

TAKRIBANI watu 21 wameuwawa katika mashambulizi kwenye kaunti mbili za mwambao wa Kenya, ambapo Jeshi la Polisi Kenya limewalaumu wanaharakati wanaotaka kujitenga katika Mkoa wa Pwani kuhusika na mashambulio hayo. Naibu Mkuu wa Polisi Kenya, Grace Kaindi alisema watu 21 wameuwawa katika mashambulizi hayo mawili ya usiku na kuwalaumu wanachama wa Chama cha Mombasa Republican Council (MRC) kundi lenye kupigania …