Pamoja na notisi iliyobandikwa tarehe 13.5.2013, ikiwataka wabomoe majengo hayo. Wakazi hao wamepuuza notisi hiyo, na sasa nyumba hizo zimekamilika na wakazi wameshahamia. Mwandishi alishuhudia nguo zikiwa zimeanikwa na ndoo zikiwa zimewekwa nje kwa ajili ya matumizi ya Kila siku. Hili ni eneo la Kigogo, pembezoni mwa mapito ya Mto Msimbazi. Eneo hilo wakati wa mvua ni ukanda wa Maji …
Mlalakuwa Mto Wetu Afya Yetu!
Bango la kuhamasisha usafi katika Mto wa Mlalakuwa, ambalo lilibeba kauli mbiu isemayo “Mlalakuwa Mto Wetu, Afya Yetu” kama lilivyonaswa na thehabari leo. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda, akizungumza chini ya daraja la Kawe Mlalakuwa kwenye kampeni hiyo ya usafi. Mkuu wa Mkoa wa Dar, Mh. Meck Sadiq nae alikuwepo katika kampeni hiyo muhimu ya usafi kwa …
Huu ni Msimu wa Miogo Tanzania, Zijue Faida zake!
Virutubisho vya muogo vinatoka kwenye madini ya zinc, iron, na magnesium, ambayo yanasaidia damu kusambaza oksijeni mwilini. Kwa kiasi kidogo cha Potassium, vyakula vilivyoandaliwa na mihogo, kwa hakika husaidia kuzuia shinikizo la damu mwilini. Majani ya Mihogo ni chanzo kizuri cha vitamini K, ambavyo vinakuza seli mwilini na kukomaza mifupa. Hizo ni faida chache tu za mihogo, kwa mujibu wa …
Wakazi wa Jangwani Waanza Kurejea Kwenye Makazi Yao Licha ya Maafa Yaliyowakuta!
Kama picha zilivyonaswa na thehabari hapo juu, inaonekana wakazi wa Jangwani wakirejesha makazi yao licha ya maafa makubwa yaliyowakuta kutokana na mvua kubwa zilizolikumba jiji la Dar hivi karibuni. Magodoro na vifaa mbalimbali vilionekana vikiwa vimeanikwa juu ya mapaa na kwingineko, tayari kuanza maisha mapya. Inasemekana serikali iliwahamishia wakazi hao eneo la Mabwepande, Manispaa ya Kinondoni, lakini inaonekana baadhi yao …
Mafuriko Ya Dar Yaleta Neema Kwa Baadhi ya Wakazi Wake!
Thehabari leo ilivinjari maeneo ya Mto Mzinga, eneo la kwa Mpalange, Manispaa ya Temeke, na kushuhudia biashara ya kuvusha watu ikiendelea kutoka upande mmoja wa Maji Kwenda mwingine. Pichani,wanafunzi (watoto)wakiwa wamebebwa na watoa huduma. Thehabari iliweza kugundua kwamba watu wazima hutozwa shillingi 500 ili kuvushwa. Uvushaji ukiendelea Wakati huo huo, vijana wengine wamebuni ajira ya kujikusanyia mchanga unaopatikana oembezoni mwa …
Mwananchi- Usifikiri Dampo, ni Kituo Cha Daladala!
Picha ya kwanza, inaonyesha chakula (mapaja ya kuku) kikiuzwa pembezoni mwa kituo cha Mabasi, Banana, wilayani Ilala. Meza zimewekwa juu ya mifereji ya kupitisha Maji ya mvua, ambayo nayo imejaa taka za aina mbalimbali. Picha ya pili ni wakazi wakipita kwa taabu juu ya Maji yenye kinyesi, baada ya baadhi wa wananchi kutumia fursa hii ya mvua kutapisha vyoo! Picha …
- Page 1 of 2
- 1
- 2