UMOJA wa Mataifa (UN) umebainisha kuwa wahamiaji wapatao 700 wanahofiwa kufariki katika kipindi cha siku tatu zilizopita katika bahari ya Mediterranean. Msemaji wa Shirika la umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi (UNHCR), Carlotta Sami, amesema mashua kadhaa zimezama katika maeneo ya kusini mwa Italia Jumatano usiku ikiwa na wahamiaji hao. Taarifa kutoka kwa baadhi ya wahamiaji waliookolewa zinaeleza kuwa juma lililopita …
Wahamiaji 400 Wazama Baharini, Korea Kaskazini Kupiga Nyuklia
WAHAMIAJI takribani 400, wengi wao wanaohisiwa kutoka nchini Somalia, wanahofiwa kuzama katika Bahari ya Mediterranean wakijaribu kuvuka kuelekea barani Ulaya. Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Misri zinasema wahamiaji hao walikuwa wakitumia boti nne kusafiria. Ndugu na jamaa wa baadhi ya wahamiaji hao wamesema baadhi ya wahamiaji hao waliokolewa na kikosi cha wana maji kutoka Ugiriki na sasa wapo nchini …
RC Awatahadharisha NIDA Juu ya Wahamiaji Haramu
Na Yohane Gervas, Rombo KUFUATIA uwepo wa wimbi kubwa la wahamiaji haramu mkoani Kilimanjaro, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa nchini (NIDA) imetakiwa kuwa makini katika zoezi la utambuzi na usajili wa watu mkoani humo kabla ya kutoa vitambulisho. Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Wilaya Moshi, Dk. Ibrahim Msengi, wakati akisoma taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidasi Gama …