SISI Wanataaluma ya Habari hapa nchini tumeamua kuungana pamoja. Lengo kubwa likiwa kusaidiana katika matatizo mbali mbali hasa ya kiafya. Muungano huu hasa umechagizwa na kuugua kwa baadhi ya wenzetu magonjwa sugu ikiwemo saratani. Tumeungana wanataaluma kutoka vyombo vya habari mbalimbali yakiwemo magazeti, Televisheni, Radio na Blogu anuai. Tuko chini ya mwamvuli wa kampeni maalum iitwayo ‘Media Car Wash for …
Hospitali ya Apollo Kuweka Kambi Kuchunguza Wagonjwa wa Moyo na Mfumo wa Fahamu Tanzania
MWEZI Machi sekta ya afya nchini Tanzania imepokea wataalam kutoka nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kutoa huduma za vipimo, ushauri na matibabu kwa Watanzania. Ujio huu umeleta faida kubwa kwa wagonjwa na wataalamu nchini. Miongoni mwa waliotembelea ni timu ya Madaktari bingwa kutoka Israel na Hospitali za Apollo zilizopo nchini India. Ziara hizi za mwishoni mwa mwezi Machi zilitanguliwa …
Wagonjwa Walazwa Chini Hospitali ya Temeke!
Bango la hospitali ya Temeke, linalo onyesha utaratibu wa kuona wagonjwa kama lilivyonaswa na Mpiga picha wetu. Ndugu ambaye hakufahamika jina lake, akiongea na mgonjwa wake, ambaye amelazimika kulala chini ndani ya wodi namba 4 kwenye hospitali hiyo ya rufaa ya mkoa wa Temeke. Uchunguzi wetu uligundua kwamba, hospitali hizi zimepandishwa hadhi mwaka jana na kuwa hospitali za rufaa za …
Mgonjwa wa Akili Aamua Kujenga Makazi Yake Nje ya Hospitali ya Magomeni!
Tatizo sio tu kwamba Mgonjwa huyo ameamua kujenga nyumba yake nje ya hospitali na Mamlaka husika kumuacha apete, bali pia nyumba yenyewe kama inavyoonekana kwenye picha, imejengwa chini ya Transfoma la Umeme! Nyumba ya Mgonjwa wa akili nje ya hospitali ya Magomeni kama ilivyonaswa na Mpiga picha wetu leo asubuhi. Picha zote na Mpiga Picha Maalum wa Thehabari