Waandamanaji Bukina faso Wachoma Bunge Kumpinga Rais

WANANCHI wa Bukina Faso wanaoendeleza maandamano wameteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, ikiwa ni hatua ya kupinga kuongeza muhula wa kutawala kwa Rais Blaise Compaore wa nchi hiyo ambaye ametawala nchi kwa miaka 27. Vituo vya Televisheni ya Taifa navyo vililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji hao kuvamia majengo ya shirika la utangazaji. Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais huku …