Vurugu za Ubaguzi Afrika Kusini; Nigeria Yaondoa Mabalozi Wake

TAIFA la Nigeria limewaita mabalozi wake waishio nchini Afrika Kusini kurejee nyumbani kufuatia mashambulizi ya kibaguzi dhidi ya wenyeji yanayofanyika Afrika Kusini. Mpaka sasa watu saba wameshapoteza uhai kufuatia mashambulizi hayo, yaliyoanza wiki tatu zilizo pita. Mali zimeharibiwa vibaya na mashambulizi hayo yamezusha hofu kubwa miongoni mwa raia wa kigeni. Balozi wa Nigeria mjini Pretoria, mji wa kibiashara na kwingineko …

Waandamanaji Bukina faso Wachoma Bunge Kumpinga Rais

WANANCHI wa Bukina Faso wanaoendeleza maandamano wameteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, ikiwa ni hatua ya kupinga kuongeza muhula wa kutawala kwa Rais Blaise Compaore wa nchi hiyo ambaye ametawala nchi kwa miaka 27. Vituo vya Televisheni ya Taifa navyo vililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji hao kuvamia majengo ya shirika la utangazaji. Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais huku …

Ukweli wa Vurugu ‘Show’ ya Diamond Ujerumani…!

UKWELI wa show ya mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kuvurugika na msanii huyo kunusurika kula kichapo mjini Stuttgart Ujerumani umewekwa wazi na muandaaji wa onesho hilo, Awin Williams Akpomiemie raia wa Nigeria. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Williams Akpomiemie ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Britts inayofanya kazi zake mjini Stuttgart Ujerumani amesema kuvurugika show hiyo kulisababishwa …