Watoto 130,000 Tanzania Wanaishi na VVU

Na Johary Kachwamba – MAELEZO TAKWIMU zinaonesha kwamba watoto 130,000 wana maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU) kati ya hao 39,317 wamefikiwa na kupatiwa huduma ya dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo. Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana wakati akifungua kongamano la nne la kitaifa la VVU na …