Na Magreth Kinabo – Maelezo RAIS Jakaya Kikwete amewataka Wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha kuwa wanasimamia Mpango Mkakati ulioboreshwa wa Kuongeza Kasi ya Kupunguza vifo vya Uzazi vya wakinamama na watoto hususan wachanga ili kutimiza malengo ya milenia namba nne na tano ifikapo mwaka 2015. Aidha Rais Kikwete aliagiza viongozi wa mapango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kuliingiza suala la afya katika mpango huo. Changamoto …