Mkuu wa Mkoa Aagiza Sheria Zitumike Kuisafisha Morogoro

Na Andrew Chimesela – Morogoro MKUU wa Mkoa wa Morogoro Dk. Rajab Rutengwe ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kutumia sheria zilizopo katika kusimamia vema suala la usafi wa mazingira. Dk. Rutengwe ametoa agizo hilo 19 Mei, 2015 wakati wa kikao maalum cha uhamasishaji wa kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira kilichofanyika katika ofisi za mkoa huo. …