Asilimia 38 ya ‘Walevi’ Kinondoni Walianza Utotoni

ASILIMIA 38 ya wanywaji wa pombe Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaa walianza matumizi ya pombe wakiwa watoto. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na Shirika la IOGT imebainika kuwa asilimia 26.5 ya watumiaji pombe walianza wakiwa watoto yaani kati ya umri wa miaka 14 hadi 17, huku asilimia 11.8 walianza …