Na Mwandishi Wetu OFISA Habari Umoja wa Mataifa (UN), Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema bado lengo la kupunguza kiwango cha umasiki lililokuwa katika malengo ya milenia yaliyomalizika mwakani litaendelea kuwa changamoto kwa nchi mbalimbali kutokana na hali ya utekelezaji wake. Bi. Nkhoma ametoa ufafanuzi huo Uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam katika Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua …
UN Yasaidia Kuokoa Maisha ya Watoto 3,000 Zanzibar
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari wa Zanzibar kwenye ofisi ndogo za mashirika ya Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar kuhusiana na mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni. Kulia ni …
Matukio Katika Picha UN Family Day
Pichani juu na chini ni baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na watoto wa wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walipojumuika pamoja mwishoni mwa juma kushiriki michezo mbalimbali kwenye UN Family Day kusheherekea maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanishwa kwake. Watoto wakifurahia kupakwa rangi usoni katika …
UN Yaipongeza Tanzania Kuwatwaa Warundi 162,156
UMOJA wa Mataifa (UN) umempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete kwa uamuzi wake wa kutoa uraia wa Tanzania kwa waliokuwa wakimbizi 162,156 wa Burundi. Pongezi hizo za UN zimetolewa Oktoba 16, 2014, na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Eneo la Maziwa Makuu, Balozi Said Djinnit wakati alipokutana na kufanya mazungumzo …
Tanzania Ipo Tayari Kiushirikiano na UN Kutekeleza MDGs
TANZANIA iko tayari kushirikiana na wanachama wote wa Umoja wa Mataifa (UN) kufikia makubaliano ya Malengo ya Maendeleo mapya baada ya Malengo ya Milenia (MDGs) ya sasa kufikia mwisho wake ifikapo mwaka 2015. Rais Kikwete amesema hayo wakati akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) jana tarehe 25 Septemba, 2014 jijini New York, Marekani. Agenda ya kikao cha Baraza …