Tanzania Yahamashisha Matumizi ya Jotoardhi Kupunguza Kero ya Umeme

Na Benedict Liwenga, Maelezo-Mbeya KUTOKANA na ongezeko la mahitaji ya nishati ya umeme nchini, nishati ya jotoardhi imetajwa kuwa ni muhimu kwa kuwa itaisaidia Tanzania kuondokana na tatizo la umeme usiokuwa na uhakika pamoja na kupunguza gharama kubwa zitokanazo na matumizi ya mitambo ya uzalishaji umeme yenye kutumia mafuta. Kauli hiyo imetolewa 8 Agosti, 2015 na Mjiolojia Mkuu toka Wizara …

Serikali Kutumia Bil 55 Kusambaza Umeme Mbeya Vijijini

  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali itatumia shilingi bilioni 55 kuvipatia umeme vijiji 244 vya mkoa wa Mbeya kupitia Miradi ya Umeme Vijijini (REA). Ametoa kauli hiyo Machi 2, 2015 wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya waliofika kusikiliza majumuisho ya ziara yake ya siku saba kwenye mkoa huo. Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mkapa, jijini …

Kijiji cha Ngareni Rombo Chaomba Umeme

WAKAZI wa Kijiji cha Ngareni Kata ya Ngoyoni Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro wameliomba Shirika la Kusambaza Umeme (TANESCO) kupelekewa huduma ya umeme jambo ambalo linawasababishia kuzorota kwa maendeleo katika kijiji hicho. Diwani wa Kata hiyo Protas Lyakurwa Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani wakati alipokua akichangia taarifa ya Shirika la kusambaza umeme iliyowasilishwa na Meneja wa TANESCO, Wilaya …