Ujumbe wa Leo!

Ujumbe wa leo kama ulivyonaswa na Mpiga picha wetu, unasema “Kazi Mbaya Uwe Nayo” , maana yake kazi utaiona mbaya kama unayo. Ukiwa huna kazi, yeyote utaiona nzuri, ili mradi mkono uende kinywani!

Ujumbe wa Leo!

Tumegundua hizi jumbe za mjini Dar huwa zinajibishana kwasababu kuna ujumbe mmoja (kwenye Bodaboda) tuliweka hapa ulikuwa unasema “Usije Mjini” na huu wa leo kwenye Bajaji unasema “Mjini Hafukuzwi Mtu” hivyo ndio viroja vya Dar! Picha na MpigaPicha Maalum wa Thehabari, Dar