Dk. Bilal Aiwakilisha Tanzania Maadhimisho ya Uhuru wa Malawi

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, Julai 06, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Malawi, sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Civo jijini Lilongwe. Katika sherehe hizo pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania, pia alihudhuria Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Waziri Mkuu wa Msumbiji na viongozi mbalimbali waliowakilisha nchi kutoka Afrika. Sherehe …