Mkurugenzi Mtendaji wa Lotus Clinic, Dialla Kassam (katikati), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya kueneza uelewa kuhusu tatizo la usonji ‘Autism’ nchini Tanzania iliyondaliwa na Lotus Medical Clinic kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na taasisi ya Autism Education Trust ya Uingereza. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama …
Ufahamu Juu ya Ugonjwa Sugu wa Figo…!
SIKU ya Figo Duniani inalenga kuongeza uelewa juu ya umuhimu wa figo zetu, afya zetu kwa ujumla na kupunguza uwepo na matokeo ya magonjwa ya figo na vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo. Katika maadhimisho ya siku hii Dk. Kavita Parihar, mkuu wa “Nephrology” na idara ya upandikizaji figo katika Hospitali ya Apollo, Ahmedabad anawatahadharisha Watanzania juu ya dalili, hatari, matatizo, …
GLAUCOMA: Mwizi wa Macho ya Watu Kimyakimya
MWEZI Januari kila mwaka Jumuiya za Kimataifa uungana ili kuongeza uelewa na kujenga ufahamu juu ya ugonjwa wa Glaucoma. Kampeni hii ya mwezi mzima inalenga kuleta tahadhari na kuelimisha juu ya chanzo, sababu na madhara ya ugonjwa huo, kampeni hii pia ulenga kuutaka umma kuchukua hatua madhubuti kabla ugonjwa huu mbaya haujasababisha athari kubwa. Kutokana na asili ya ugonjwa huu …
Baraza la Mawaziri Lilinikataza Kutaja Ugonjwa – Rais Kikwete
Na Mwandishi Wetu, RAIS Jakaya Kikwete amewasili salama nchini Tanzania leo akitokea nchini Marekani alipokuwa kwa matibabu ambapo alifanyiwa upasuaji kutibiwa saratani ya tezi dume katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore, Maryland. Akizungumza na wanahabari mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam alisema alipokuwa akiliarifu Baraza lake la …
Hizi Ndizo Sababu za Ugonjwa wa Kisukari….!
SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) kwa kushilikiana na Shirika la kisukari kimataifa la International Diabetes Federation (IDF) walianzisha Siku ya Kisukari Duniani mnamo mwaka 1991 ili kuadhimisha kuzaliwa kwa mwanasayansi Frederick Banting ambaye kwa kushirikiana na Charles Best aligundua tiba muhimu kwa wagonjwa wa kisukari ya insulin mnamo mwaka 1922. Novemba 14 Kila mwaka mashirika ya kiserikali, mashirika binafsi, wagonjwa …
Utoaji Chanjo ya Surua na Rubella Ilala Wavuka Lengo
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO MANISPAA ya Ilala imevuka lengo la kutoa chanjo ya ugonjwa wa Surua na Rubella kwa watu 468,297 ambapo awali lengo lao lilikuwa kutoa chanjo hiyo kwa watu 445,801 wakati wa wiki ya kutoa chanjo hiyo nchini. Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Ilala Dk. Willy Sangu leo jijini Dar es salaam alipokuwa akitoa …