Rais Museveni, Magufuli Wasaini Utekelezaji Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi

    RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, leo tarehe 21 Mei, 2017 wametia saini tamko la pamoja (Communiqué) la kukamilika kwa majadiliano ya vipengele vya mkataba ambao utasainiwa baadaye kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini …

Mpinzani wa Museven, Besigye Aeleza Alivyovyanyaswa na Polisi

KIONGOZI wa upinzani nchini Uganda Kiiza Besigye ameliambia shirika moja la habari Kuwa alitiwa mbaroni na polisi nchini humo mara nne kwa muda wa siku sita kufuatia uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita. Licha ya mshikemshike alioupata matokeo ya uchaguzi huo yalimpa ushindi Rais Yoweri Museven kutawala nchi hiyo kwa muhula wa tano mfululizo. Bw. Besigye ambaye yupo kizuizini nyumbani kwake kwa …

Yoweri Museveni Atangazwa Mshindi wa Urais Uganda

TUME ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa ni mshindi wa Uchaguzi wa Urais uliofanyika Alhamisi iliyopita. Kwa mujibu wa tume hiyo Rais Museveni alipata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dk. Badru Kiggundu. Mpinzani wake mkuu Dk. Kizza Besigye alipata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia …

Boniface Mkwasa Kutupa Karata ya Kwanza Dhidi ya Uganda

TIMU ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kuondoka nchini siku ya alhamis kuelekea nchini Uganda kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaofanyika siku ya jumamosi nchini humo. Mchezo huo wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN 2017 zitakazofanyika nchini Rwanda utachezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Nakivubo jijini Kampala kuanzia …