UCHAGUZI Mkuu wa Tanzania wa mwaka 2015 uliokuwa na historia ya pekee kiushindani umemalizika tangu Oktoba 25, 2015. Kinachofanyika hivi sasa ni Serikali iliyoshinda chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuunda Serikali maeneo mbalimbali ili iweze kuwatumikia wananchi kwa miaka mitano na hasa kutekeleza miongoni mwa ahadi iliyozitoa kwa wapiga kura wake. Pamoja na hayo, yapo mambo kadhaa ambayo …
NEC Yatangaza Kumalizika Kibali cha Waangalizi wa Uchaguzi
KUHUSU KUMALIZIKA KWA KIBALI CHA WATAZAMAJI WA UCHAGUZI MKUU WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI MWAKA 2015 Kwa mujibu wa Kifungu cha 63 (4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa mamlaka ya kuandaa na kutoa mialiko kwa Watazamaji wa Uchaguzi wa Ndani na Nje ya Nchi. Ili kuweza kutekeleza matakwa ya kisheria, …
Wajue Wabunge Watatu Walioshinda Kura Nyingi Zaidi
Wajue Wabunge Watatu Walioshinda Kura Nyingi Zaidi 1) Joseph Osmund MBILINYI (CHADEMA) toka JIJI LA MBEYA Jimbo la MBEYA MJINI alipata jumla ya kura 108,566 2) Ally Mtolea ABDALLAH (CUF) toka JIJI LA DAR ES SALAAM Jimbo la TEMEKE aliyepata jumla ya kura 103,231 3) Abdul-Aziz Mohamed ABOOD (CCM) toka MANISPAA YA MOROGORO Jimbo la MOROGORO MJINI jumla ya kura …
Joto la Kisiasa Laanza Kupanda Rombo
JOTO la siasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwishoni mwa mwaka huu limeanza kupanda wilayani Rombo baada ya mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Fraterni Michael Lasway kutangaza nia ya kugombea Jimbo la Rombo kupitia tiketi ya chama hicho. Lasway ambaye kwa sasa ni Ofisa Manunuzi kutoka Hospitali ya Aga Khani ya jijini Dar es Salaam ametangaza uamuzi huo wakati alipozungumza na …
Upinzani Watoa Masharti Magumu Kushiriki Uchaguzi Mkuu 2015
SERIKALI imetakiwa kuandaa taratibu za mpito za kushughulikia Uchaguzi Mkuu ujao ili kunusuru nchi kuingia katika mtanziko unaoweza kuwa chanzo cha machafuko ya kisiasa, endapo utafanyika bila kupatikana kwa Katiba Mpya la sivyo Kambi Rasmi ya haitashiriki. Hayo yalielezwa jana na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alipokuwa akitoa hotuba ya kambi hiyo bungeni kuhusu Makadirio ya …