Benki ya Posta Yawafunda Wafanyabiashara Tunduma

BENKI ya Posta Tanzania (TPB), Tawi la Tunduma imetoa mafunzo kwa wajasiriamali wa Tunduma, wilayani Momba. Semina hiyo iliyohudhuriwa na wajasiriamali wapatao 100, ililenga kuwaelimisha wafanyabiashara hao kuhusu matumiza mazuri ya huduma za kibenki, hususan mikopo inayotolewa na benki hiyo. Akifungua semina hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiudy Saideya, aliipongeza Benki ya Posta kwa kutoa mafunzo ambayo alisema yanawasaidia …