NEC Yatangaza Tarehe za Uchaguzi wa Ubunge na Udiwani Uliohairishwa

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza tarehe za Uchaguzi wa Ubunge na Udiwani katika Jimbo na Kata ambazo hazikufanya Uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Octoba 2015 kwa sababu mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan K. Kailima imezitaja tarehe hizo kuwa ni tarehe 15 Novemba na tarehe 13 …

NEC Yawaondoa Hofu Wananchi Juu ya Wizi na Udanganyifu wa Kura

Na Ismail Ngayonga, MAELEZO TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitoa wasiwasi vyama vya siasa kuwa hakutakuwepo na wizi na udanganyifu wa kura katika matokeo ya uchagauzi wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajia kufanyika nchini tarehe 25 Oktoba, mwaka huu. AIdha NEC imesema ipo tayari kushirikiana na wataalamu wa vyama hivyo katika kubaini vyanzo vya wizi wa kura iwapo tatizo …

Tume ya Uchaguzi Yatoa Tahadhari kwa Viongozi wa Dini

TUME ya Taifa ya uchaguzi NEC imewaomba viongozi wa dini zote kutumia majukwaa yao kuwaelimisha wapiga kura bila kuonyesha hisia za kuegemea upande wowote wa mgombea ili waweze kufanya maamuzi sahihi wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva kwenye Mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam uliowakutanisha wadau hao wa uchaguzi na …

Mkurugenzi Mpya wa Tume ya Uchaguzi Aapishwa na Rais

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mabadiliko ya Utendaji katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kumteua Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi. Aidha, Rais Kikwete amemteua Jaji Richard Mziray kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vile vile, Rais Kikwete amewateua majaji wapya 13 wa Mahakama …

Tume ya Uchaguzi Yatoa Ratiba ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) imetangaza rasmi ratiba ya Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 2015. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Jaji wa Rufaa Damian Lubuva uteuzi wa nafasi za wagombea unatarajiwa kuanza Agosti 21, 2015 vyama vyote vya siasa. Taarifa hiyo imesema uteuzi wa nafasi hizo …