Ibada ya Kumuombea Marehemu Amin Elias Mbaga Dar

ilia na familia ya Marehemu Amin Elias Mbaga wakishiriki misa ya kumuombea aliyekuwa mfanyakazi mwenzao, marehemu Amin Elias Mbaga. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana kuelekea Kilimanjaro kwa mazishi.[/caption] Marehemu Amin Elias Mbaga aliyekuwa Meneja Uhusino alifariki Oktoba 13, 2014 katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam. Na ibada ya kumuombea imefanyika Kanisa la KKKT Sinza Kumekucha kabla ya kusafirisha …

TTCL Yaanzisha Kituo cha Intaneti ‘IP Pop’ Tanzania

KAMPUNI ya Simu nchini Tanzania (TTCL) imeanzisha kituo cha kuuzia huduma za interneti ‘IP Pop -Internet Protocol Point of Presence’ nchini ikiwa ni jitihada za kuboresha huduma za mawasiliano zaidi. Huduma kama hii awali ilikuwa ikinunuliwa nje hasa makampuni anuai yanayotoa huduma hizo barani ulaya. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mkuu Mauzo na Masoko wa …

Tangazo Msiba wa Amin Elias Mbaga wa TTCL

MENEJIMENTI ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) inasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzao, Amin Elias Mbaga aliyekuwa Meneja Uhusino kilichotokea tarehe 13.10.2014 katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam. Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza Kumekucha Ibada ya kumuombea marehemu itafanyika tarehe 15/10/2014 katika Kanisa la KKKT Sinza Kumekucha kuanzia saa saba mchana na baada ya ibada …

TTCL Yazinduwa Bonanza la SHIMMUTA Dar

OFISA Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura Oktoba 11, 2014 amezinduwa Bonanza la Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) lililofanyika viwanja vya Chuo Kikuu (UDSM) jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika hotuba yake, iliyosomwa kwa niaba na Ofisa Mkuu wa Biashara wa TTCL, Kanda ya Dar es Salaam, Karim …