TFF Yataja Timu Zitakazo Shiriki Mapinduzi

TIMU za Azam, Mtibwa Sugar, Simba na Yanga zitashiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayofanyika kisiwani Zanzibar kuanzia Januari 1 hadi 13 mwakani. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ruhusa kwa timu hizo kucheza mashindano hayo baada ya kuhakikishiwa na Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kuwa kesi iliyofunguliwa dhidi ya viongozi wake imeondolewa mahakamani.   Kutokana …

Mkutano Mkuu TFF Kufanyika Singida, Mfuko wa Maendeleo…!

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepanga Mkutano Mkuu wa Kawaida wa mwaka ufanyike Machi 14 na 15 mwakani mjini Singida.   MGOGORO NDANI YA ZFA Kamati ya Utendaji imepokea kwa masikitiko taarifa za masuala ya mpira wa miguu Zanzibar kupelekwa mahakamani. Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kitendo hicho …

TFF Yaifuata CRDB, Yafanya Marekebisho ya Katiba

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana Desemba 19 mwaka huu jijini Dar es Salaam, imezingatia upungufu uliopo katika utekelezaji wa matumizi ya tiketi za elektroniki.   Hivyo, Kamati hiyo imeiagiza Sekretarieti ya TFF kuwasiliana na benki ya CRDB inayoendesha mfumo huo wa matumizi ya tiketi za elektroniki kuhusu upungufu huo na kuhakikisha unafanyiwa kazi. …

TFF Yatangaza Rasmi Ligi ya Wanawake, Proin Promotions Yadhamini

 Rais Wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akizungumza na wanahabari leo katika ofisi za TFF kuhusu kampuni ya Proin Promotions Ltd kudhamini Mashindano ya mpira wa miguu kwa wanawake yajulikanayo kama Kombe la Wanawake Taifa, mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 28 Disemba kwa kushirikisha timu kutoka Mikoa yote ya Tanzania. Mashindano hayo yatazinduliwa Mkoani Mwanza kwa …

TFF Yaomba Usajili wa Copa Coca-Cola 2014

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeitaka mikoa mitano kuwasilisha usajili wa wachezaji wake kwa ajili ya mashindano ya Taifa ya Copa Coca-Cola 2014 kabla ya Desemba 5 mwaka huu. Mikoa hiyo ambayo haijawasilisha usajili wake hadi sasa kwa ajili ya michuano hiyo inayoanza Desemba 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam ni Arusha, Dodoma, Katavi, Kusini Pemba, Kusini …

TFF, Wanahabari Wawalilia Munyuku na Karashani

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko vifo vya waandishi wa habari Innocent Munyuku na Baraka Karashani vilivyotokea Novemba 19 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Wakati TFF ikitoa tamko la rambirambi waandishi wa habari mbalimbali wameoneshwa kuguswa na kifo cha ghafla cha mwanahabari Mnyuku pamoja na kile cha mwanahabari Karashani kilichotokea akipatiwa matibabu juzi katika Hospitali …