TFF Yarejesha Ofisi Karume, Muda wa Usajili Waongezwa

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeamua kurejesha ofisi zake Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kwa vile mipango ya uendelezaji wa eneo hilo bado haijakwenda kama ilivyopangwa awali.   Uendelezaji wa eneo utafanyika wakati ofisi zikiwa hapo hapo, na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) litasaidia katika uendelezaji huo utakaofanyika kwa awamu. Vilevile FIFA imeahidi kusaidia uboreshaji …