Benki ya TPB Yachangia Madawati Serengeti

    BENKI ya Posta Tanzania (TPB) imetoa mchango wa madawati na viti 50 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni Nane kwa Shule ya Sekondari ya Ikoma, iliyopo Wilayani Serengeti Mkoani Mara. Mchango huo wa madawati ulikabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu na Afisa Mtendaji Mkuu wa (TPB) Sabasaba Moshingi, kwenye hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo. …