Bodi ya Filamu Tanzania Yakomalia Sheria, Kanuni

Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM BODI ya Filamu Tanzania imezitaka Kampuni za filamu nchini kufuata Sheria na Kanuni mbalimbali wakati wa kutengeneza filamu ili kuepusha ukiukwaji wa Sheria na Kununi. Rai hiyo imetolewa leo na Katibu wa Bodi hiyo, Bi. Joyce Fissoo wakati alipofanya mkutano na Kampuni ya Kajala Entertainment ambapo mnamo Septemba 22, mwaka huu ilikagua Filamu fupi ya kampuni …

Wamiliki wa Blogu Tanzania Wateua Kamati ya Muda Kuongoza…!

WAMILIKI wa Mitandao ya Kijamii Tanzania wameteua viongozi wa muda ambao watafanya kazi ya kushughulikia usajili wa Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya kijamii (Bloggers) ili kuwaunganisha waendeshaji wa mitandao hiyo ya kijamii Tanzania. Uteuzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mlimani City kwenye mkutano wa mafunzo ulioandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) …

Washindi 100 Kuzawadiwa SamSung Gear S, Kifaa cha Galaxy Note 4

KAMPUNI ya vifaa vya kieletroniki ya Samsung imezindua kampeni ya kuweka oda kwabidhaa yake mpya ya Galaxy Note 4 nchini Tanzania, ikiwa ni sehemu ya kushamirisha uzinduzi mkubwa utakofuatia wa bidhaa inayosubiriwa kwa shauku ya Samsung Galaxy Note 4. Kampeni hiyo itakayoendeshwa kuanzia tarehe 31 Oktoba hadi14 Novemba 2014, inadhamiria kuwapa wateja wake wakudumu nafasi ya kujipatia bidhaa hiyo ya …

JK Awapasulia Watumishi wa Umma Tanzania

Na Mwandishi Maalum, RAIS Jakaya Kikwete amewataka watumishi wa umma nchini kubadilika katika utendaji wao ili kuwa wawezeshaji zaidi badala ya wakwamishaji katika kutoa maamuzi yanayopelekea utendaji wa shughuli mbalimbali nchini. Rais Kikwete ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 10 ya Tume ya Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam. “Watu wanaona utumishi wa Umma …

Matukio Picha Siku Ilipofanyika ‘Ndoa’ ya UKAWA

VYAMA vinne vya upinzani nchini, ambavyo ni Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na NLD vilisaini makubaliano ya kushirikiana pamoja na kusimamisha mgombea mmoja katika chaguzi zote zijazo kwa mwaka 2014. Vyama hivyo vimeibuka na nguvu mpya baada ya kuunganishwa na hoja ya kutetea Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ilielezewa kuwa ilitokana na maoni ya …