WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameuagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuboresha Idara ya Mipango na Usanifu katika wakala huo ili kupata matokeo mazuri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini. Prof. Mbarawa ameutaka wakala huo kuboresha kanuni zinazosimamia aina ya vyombo vya moto vinavyotumia barabara zote nchini ikiwemo ili kuweza kusaidia miundombinu hiyo kudumu …
Prof. Mbarawa Akemea Hujuma Miundombinu ya Barabara Singida
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amewaagiza viongozi wa Serikali kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama na wananchi mkoani Singida kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria wananchi wanaohujumu miundombinu ya barabara na kuisababishia hasara Serikali. Profesa Mbarara ametoa agizo hilo mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilomita 89.3 kwa kiwango …
Wafanyakazi wa Mizani Watakiwa Kuonesha Uwazi, Uadilifu na Weledi
WAFANYAKAZI wa Mizani hapa nchini wametakiwa kufanya kazi kwa uwazi, uadilifu, na weledi ili kuzingatia sheria zinazoongoza sekta hiyo na hivyo kutenda haki kwa wasafirishaji wote na kujenga taswira nzuri kwa taasisi hiyo. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Julias Chambo katika mafunzo kwa maofisa waendesha mizani hapa nchini yanayofanyika …
Serikali Haitawavumilia Wazembe: Waziri Prof. Mbarawa
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa amemtaka mkandarasi anayejenga barabara ya Mwenge – Moroco KM 4, kuhakikisha inajengwa kwa ubora uliokusudiwa na kukamilika kwa wakati ili kumaliza adha ya msongamano wa magari katika eneo hilo. Akikagua ujenzi wa barabara hiyo Prof. Mbarawa amemtaka Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha ujenzi huo …