Asilimia 38 ya ‘Walevi’ Kinondoni Walianza Utotoni

ASILIMIA 38 ya wanywaji wa pombe Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaa walianza matumizi ya pombe wakiwa watoto. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na Shirika la IOGT imebainika kuwa asilimia 26.5 ya watumiaji pombe walianza wakiwa watoto yaani kati ya umri wa miaka 14 hadi 17, huku asilimia 11.8 walianza …

TAMWA Yashauri Taifa Liwekeze kwa Watoto

CHAMA cha Wanahabari Wanawake nchini Tanzania (TAMWA) kimeitaka Serikali na jamii kwa ujumla kuwekeza katika kumuandaa mtoto kwani licha ya kuwa zawadi kubwa, watoto pia ni tumaini na uhai wa taifa kuendelea. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka katika taarifa iliyosomwa kwa wanahabari jijini Dar es Salaam kuhamasisha jamii kwa ujumla kuwajali watoto hasa kwenye …