Wanahabari Waliminya Sauti za Wanawake Uchaguzi Mkuu – TAMWA

Na Mwandishi Wetu CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimesema wanawake waliogombea nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 walikosa nafasi ya kutosha kuzungumza kwenye vyombo vya habari. Alisema utafiti mdogo walioufanya katika vyombo vya habari kadhaa ulibaini kuwa ni asilimia 11 tu ya wanawake wagombea ndio walipata nafasi ya kuandikwa katika magazeti wakati wa uchaguzi huo. Takwimu hizo …

TAMWA Kuwajengea Uwezo Waandishi Uandishi Habari za Uchaguzi

CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kimepanga kuwajengea uwezo baadhi ya waandishi wa habari nchini juu ya uandishi wa habari za uchaguzi kujiandaa na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2015. Akizungumza katika mkutano na baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Gradness Munuo alisema mafunzo hayo yatawaongezea ujuzi …

Mtandao wa Wanawake na Katiba Waeleza Sababu za Kuunga Mkono Katiba Inayopendekeza

MTANDAO Wanawake na Katiba nchini pamoja na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) wamesema wanaunga mkono Katiba iliyopendekezwa na kujivunia hatua waliopiga katika kudai haki mbalimbali za mwanamke kwenye Katiba hiyo ukilinganisha na ile ya Mwaka 1977. Mtandao huo umetoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuzungumzia hatua ambayo mtandao huo …

TAMWA Yazinduwa Tathmini ya Ripoti Mradi wa GEWE

CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na taasisi anuai za kijamii kimezinduwa tathmini ya ripoti juu ya utekelezaji wa mradi wa Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE). Akizinduwa ripoti hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka alisema mradi huo …