Utoaji Chanjo ya Surua na Rubella Ilala Wavuka Lengo

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO MANISPAA ya Ilala imevuka lengo la kutoa chanjo ya ugonjwa wa Surua na Rubella kwa watu 468,297 ambapo awali lengo lao lilikuwa kutoa chanjo hiyo kwa watu 445,801 wakati wa wiki ya kutoa chanjo hiyo nchini. Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Ilala Dk. Willy Sangu leo jijini Dar es salaam alipokuwa akitoa …