Kocha Mkuu Stars Kutimuliwa, Apewa Mtihani wa Mwisho…!

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) imesikitishwa na mwenendo mbovu wa Taifa Stars, hivyo kumpa mtihani wa mwisho kocha mkuu wa timu ya Taifa, Mart Nooij na endapo atashindwa atafukuzwa kazi. Kwa mujibu wa taarifa ya kamati hiyo mtihani aliopewa kocha Mart Nooij ni kuhakikisha anafuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) …

TFF Kuchunguza Hujuma ya Stars, Yanga Yatakiwa Kuwasilisha Rasimu

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa zilizoandikwa kwenye baadhi ya Vyombo vya Habari zikielezea tuhuma za hujuma kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) katika mechi za kufuzu mashindano ya AFCON.   TFF pamoja na kutokuwa na uthibitisho wa tuhuma hizi nzito haliwezi kuzikalia kimya. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania litateua jopo la kuchunguza …