TFF Yapongeza Mali, Soka la Ufukweni Kambini

RAIS wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini –TFF Bw. Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa Rais Boubacar Diara wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Mali (FMF) kwa kutwaa Ubingwa wa Afrika kwa vijana U17. Katika salam zake mh. Malinzi amesema mafanikio mazuri waliyoyapata  FMF yametokana na uongozi bora, kamati ya utendaji na mipango thabiti waliyoiweka katika soka …