Mgogoro: TFF Yawaita Simba na Singano

YAH: MGOGORO KATI YA MCHEZAJI RAMADHAN SINGANO NA KLABU YA SIMBA. TFF imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mgogoro wa kimkataba kati ya Mchezaji Ramadhani Singano wa klabu ya Simba. TFF imeagiza mwakilishi wa klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Simba wafike ofisi za TFF siku ya Jumanne tarehe 09/06/2015 kwa mazungumzo. Kila upande umetakiwa uje na vielelezo vyake. …