Maambukizi ya Ebola Yaongezeka Sierra Leone

SHIRIKA moja la hisani limesema licha ya uhaba mkubwa wa vituo vya afya nchini Sierra Leone, kiwango cha visa vitano vya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola kinatokea kila saa nchini humo. Shirika la Kimataifa linalohudumia watoto (Save the Children) linasema kuna jumla ya visa 765 vipya vya Ebola ambavyo vimeripotiwa katika taifa hilo la Afrika Magharibi huku kukiwa kuna vitanda …