Mbunge Halima Mdee Mikononi mwa Polisi Dar…!

  HATIMAYE Jeshi la Polisi Dar es Salaam limemkamata Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) ikiwa ni kuitikia amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Alli Hapi. Taarifa zinasema mbunge huyo, alikamatwa na Jeshi la Polisi nyumbani kwake Makongo Juu na anashikiliwa na Kituoni cha Polisi Oysterbay. Kiongozi wa CHADEMA (Katibu) wa Dar es Salaam, Henry Kilewo ametoa taarifa za …

Masikini Mdee, Polisi Waagizwa Kumkamata Saa 48

  MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Ally Hapi amelitaka Jeshi la Polisi Tanzania, kumtia ndani Mbunge wa Kawe, Bi. Halima Mdee kwa kile alichodai katoa kauli ya kumtusi, dhihaka na uchochezi kwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli katika kauli yake aliyoitoa kwa waandishi wa habari. DC Hapi alisema kauli za mbunge huyo aziwezi kuvumiliwa hivyo …

Nape Aonja Joto ya Jeshi la Polisi, Wamzuia Kuzungumza na Wanahabari…!

  ALIYEKUWA Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Mnauye leo ameonja joto la jiwe la Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam baada ya kumzuia kuzungumza na vyombo vya habari alipotaka kuzungumza yamoyoni baada ya kuvuliwa nafasi yake ya uwaziri. Jeshi la Polisi lilizuia waandishi wa habari kuingia katika Hoteli ya Protea ya jijini Dar es Salaam sehemu …

CCM ni Chuki Visasi…Wapinzani Wakitimuana ‘Wanafukuza Waasi, Wasaliti’

Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini JUMAMOSI ya Machi 11, 2017 Chama cha Mapinduzi (CCM) ‘kiliondoa woga’ na kufanya jambo ambalo halikutarajiwa na wengi nchini baada ya kuwatimua baadhi ya wanachama na kuwavua uongozi wengini huku baadhi yao wakisimamishwa na wengine wakionywa, MaendeleoVijijini inaripoti. Waliofukuzwa uanachama ni pamoja na mwanachama mkongwe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Sophia Simba ambaye amepoteza rasmi nafasi yake ya Ubunge wa …

Shibuda Awataka Watanzania Kumuunga Mkono Rais Magufuli

 Mkutano ukiendelea.  Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo. Mwanahabari Suleiman Msuya akiuliza swali katika mkutano huo.   Na Dotto Mwaibale   WATANZANIA wameombwa kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli kwa jitohada zake anazozifanya za kuongoza nchi. Mwito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini John Shibuda wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kuuaga …

Diwani Chadema Atupwa Lupango kwa Kukiuka Maadhimio

Na Mathias Canal, Singida JESHI la Polisi Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida limemtia nguvuni Diwani wa Kata ya Iseke kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Emmanuely Njingu kwa kosa la kukwamisha shughuli za serikali kwa kuzuia watendaji wa serikali kufanya kazi yao ikiwemo ukusanyaji wa mapato. Njingu ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya fedha awali kabla ya …