RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Uteuzi wa Masaju ulianza Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam. Kabla ya uteuzi wake, Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya …
Serikali Yaanza Kujibu ‘Escrow’ Bungeni, Yadai PAC Imedanganya…!
SERIKALI imeanza kujibu hoja za tuhuma za uwepo wa uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow takribani sh. bilioni 306 zinazodaiwa kuchotwa na watu binafsi, viongozi wa siasa, watendaji wa Serikali pamoja na viongozi wa dini, kwa mujibu wa ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyowasilishwa jana bungeni mjini Dodoma. Akijibu hoja hizo leo mjini …
Serikali, Sekta Binafsi Kuwezesha Wasomi Kujiajiri…!
Na Eleuteri Mangi- Dodoma SERIKALI imesema inaendelea kushirikiana na sekta binafsi kuweka mazingira rafiki kwa kuboresha mifumo ya ajira katika sekta ya umma na ile ya binafsi ili kujenga uchumi wa kisasa unaozalisha ajira pamoja na kuwawezesha vijana wasomi nchini kujiajiri. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janet Mbene kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Saada …
Akaunti ya Escrow Yamtesa Pinda Bungeni, Wabunge Wacharuka
Na Joachim Mushi TUHUMA za uchotaji wa fedha Dola za Marekani milioni 200 katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyotua bungeni imeendelea kuitesa Serikali huku kukiwa na kila dalili ya kuibuka mazitoka katika tuhumwa hizo. Leo mjini Dodoma wabunge mbalimbali wamechachamaa na kuungana kwa pamoja wakitaka ripoti ya uchunguzi huo iwasilishwe bungeni ili wabunge waijadili na kuitolea uamuzi. Hali ya kuibuka …
Serikali Ichukue Hatua Kupunguza Uhaba wa Dawa
TUNASIKITISHWA na namna ambavyo serikali imekuwa ikishughulikia suala laupungufu wa dawa na vifaa tiba nchini. Siku za karibuni, kumekuwepo na taarifa za ukosefu wa dawa na vifaa tiba katika sehemu mbalimbali nchinilakini serikali bado haijachukua hatua madhubuti, jambo ambalo linaweza kuchangia wagonjwa kuteseka zaidi na hata kusababisha vifo. Sikika ilitegemea serikali ingeangalia janga hili kwa makini zaidi na kulipa mara …
Serikali Kupunguza Maambukizi ya Ukimwi Hadi Sifuri
Na Genofeva Matemu – Maelezo SERIKALI imepanga mikakati na kusimamia juhudi zinazofanywa na kuendelezwa na wadau wa ukimwi kuhakikisha kuwa maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi yanapungua hadi kufikia sifuri ifikapo mwaka 2025. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Fatma Mrisho wakati wa mkutano wa Serikali na wadau wa ukimwi kupitia utekelezaji …