Na Frank Mvungi, MAELEZO SERIKALI imeendelea kuimarisha umoja, amani na utulivu miongoni mwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha miaka kumi. Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Angelina Madete wakati wa mkutano na vyombo vya habari jijini Dar es salaam. Mhandishi Madete alisema kuwa suala la muungano ni miongoni mwa …
Serikali Yahaidi Neema; Tuzo za Filamu 2015
SERIKALI imesema itaendelea kuweka mfumo mzuri na kujenga mazingira mazuri ili kuhakikisha biashara ya filamu inaimarika, ikiwa ni pamoja na kuwavutia wawekezaji binafsi waliopo tayari kuwekeza katika tasnia ya filamu. Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi wa Tuzo za Filamu 2015, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala alipokuwa akihutubia wakati wa …
Uwazi na Uwajibikaji Unawahusu Wote si Serikali tu-JK
Na Joachim Mushi RAIS wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema dhana ya uwazi na uwajibikaji haipaswi kutekelezwa na Serikali pekee, bali inawahusu pia waendeshaji wa asasi za kiraia ili kujenga imani kwa raia wote. Rais Kikwete amebainisha hayo katika hotuba yake kwenye Mkutano wa Open Government Partnership (OGP) uliofanyika jijini Dar es Salaam. Alisema dhana ya uwazi na uwajibikaji inawahusu wadau …
Elimu Inayotolewa Sasa Inamuandaa Mwanafunzi Kujitegemea- Serikali
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya kukutana na wadau wa elimu walioshiriki mkutano wa kutathmini sekta …
Serikali Kubeba Gharama za Msiba wa Brigedia Hashim Mbita
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mtumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Wananchiwa Tanzania (JWTZ) na Chama cha TANU na Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika kwa miaka mingi, Brigedia Hashim Mbita. Mzee Mbita ambaye amekuwa anauguza afya yake kwa muda sasa amefariki asubuhi ya leo, …
Serikali Yaandaa Sheria Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu – Mwanasheria Mkuu
SERIKALI imesema inaandaa mswada wa sheria ambayo itawalinda watoaji wa taarifa za masuala ya uhalifu ikiwa ni jitihada za kuimarisha mapambano dhidi ya vitendo mbalimbali vya uhalifu nchini Tanzania. Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. George Masaju alipokuwa akitoa vyeti kwa baadhi ya waandishi wa habari waliokuwa katika mpango wa …