Waziri Mbarawa Ataka Mfuko wa Mawasiliano Kuwafikia Wanavijiji

    WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Menejimenti ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF), kuhakikisha vijiji vyote nchini ambavyo havijaunganishwa na huduma ya mawasiliano vinaunganishwa kabla ya mwisho wa mwaka huu. Aidha, Profesa Mbarawa amesisitiza mfuko huo kutoa kipaumbele kwa vijiji vyote vilivyomo sehemu za mipakani ili kuimarisha ulinzi na uharaka wa mawasiliano katika …

Wadau wa Sekta ya Barabara na Reli Watakiwa Kuchangamkia Fursa

  WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa sekta ya miundombinu ya Reli na Barabara kushirikiana na Serikali katika kuchangamkia fursa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya sekta hiyo hapa nchini. Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Saba wa wadau wa Sekta hiyo, Prof. Mbarawa amesema kwa sasa …

Oracle Sytem Yakusudia Kuwekeza Tanzania

KAMPUNI ya Oracle Sytem Limited kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano itakuwa na mkutano wa The Africa Security Summit utakaofanyika hoteli ya Kilimanjaro, Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2016. Lengo la mkutano huu ni kuwakutanisha wadau na wataalamu mbalimbli wa Taasisi za Serikali na sekta binafsi wapatao watu 200 kutoka ndani na nje ya nchi. Mkurugenzi …

Waziri Ataka ‘Data Centre’ ya TTCL Ianze Kazi, Atoa Mwezi Mmoja…!

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametoa mwezi mmoja kwa Katibu Mkuu wa Wizara anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini (TTCL), kuhakikisha kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kilichopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam kinaanza kufanya kazi. Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo kufuatia kukamilika kwa Data Centre hiyo miezi kadhaa iliyopita …