TaSUBa Yaombwa Kufunza Sanaa na Utamaduni Afrika Mashariki

  Benjamin Sawe, Bagamoyo   TAASISI ya Sanaa Bagamoyo imeaswa kuendelea kutoa mafunzo ya sanaa na utamaduni ambayo yatakidhi mahitaji ya soko kwa nchi za Afrika Mashariki.   Hayo yamesemwa na Makongoro Nyerere kwa niaba ya Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Margaret Ntantongo Zziwa katika Ufunguzi wa Tamasha la 33 la sanaa na utamaduni wa Mtanzania lililofanyika katika Taasisi hiyo …