Ofisa Uhusiano wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Jafarri Malema (kushoto), akizungumza na wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu shughuli zinazofanywa na Rita na umuhimu wa cheti cha kuzaliwa. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Rita, Grace Kyasi. Wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo wakiwasikiliza maofisa wa Rita walipokuwa wakizungumza nao. …
RITA na Mafanikio ya Mkakati wa Usajili wa Utoaji wa Vyeti vya Kuzaliwa
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM. MOJA YA MAJUKUMU makubwa ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kama taasisi ya Serikali iliyopo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria ni kuratibu na kusimamia usajili wa vizazi na vifo nchini. Cheti cha kuzaliwa hutolewa kwa mwananchi mara baada ya kusajiliwa kwani cheti hicho ni nyaraka muhimu na kisheria ndiyo pekee inayotakiwa kuthibitisha …
Wanafunzi 15,120 Wapewa Vyeti vya Kuzaliwa Ilala
Na Fatma Salum, Maelezo JUMLA ya wanafunzi 15,120 wa Shule za Msingi na Sekondari katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameweza kusajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa kupitia Mkakati wa Usajili na Kutoa Vyeti vya Kuzaliwa unaotekelezwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA). Hayo yamesemwa na Meneja Masoko, Mawasiliano na Elimu kwa Umma kutoka Wakala wa …