JK Atuma Rambirambi Vifo vya Mvua ya Mawe Shinyanga

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ali Nasoro Rufunga kuomboleza vifo vya watu 38 huku wengine 82 wakijeruhiwa usiku wa kuamkia tarehe 4 Machi, 2015. Tukio hilo la kusikitisha limetokea katika Kata ya Mwakata iliyoko katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kufuatia mvua kubwa ya mawe …

JK Atoa Pole Vifo vya Wanafamilia Ajali ya Moto

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi za dhati ya moyo wake kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiq kuomboleza vifo vya watu sita wa familia moja waliopoteza maisha kwa moto usiku wa kuamkia, Januari 7, 2015, katika eneo la Kipunguni A, Ukonga Banana, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa …

Rais Kikwete Amtumia Rambirambi Rais Mpya wa Mozambique, Nyusi

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Rais mpya wa Mozambique, Filipe Jacinto Nyusi salamu za rambirambi kuomboleza vifo vya watu 79 waliopoteza maisha yao kutokana na kunywa pombe yenye sumu. Aidha, Rais Kikwete amewatakia watu wengine 174 ambao wamepata madhara ya viwango mbali mbali katika tukio hilo, baadhi yao bado wamelazwa hospitali, kupata nafuu ya …

JK Atuma Rambirambi Kifo cha Mtangazaji Ben Kiko

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dk. Fenela Mukangara kuomboleza kifo cha aliyekuwa Mtangazaji na Mwandishi Mkongwe na Mahiri hapa nchini wa iliyokuwa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo kwa sasa ni TBC Taifa, Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kiko. Ben Kiko …