Rais Zuma Awatembelea Raia wa Kigeni Wanaoshambuliwa Afrika Kusini

RAIS Jacob Zuma amewatembelea watu walioathirika na ghasia hizo, mauwaji pamoja na kuibwa kwa mali zao huku akiahidi kukabiliana vilivyo na wimbi la mashambulio hayo. Bwana Zuma alifutilia mbali ziara yake nchini Indonesia, ili kukabiliana na vurumai hizo zilizoanza majuma mawili yaliyopita. Amesema kuwa ghasia hizo ni kinyume na maadili ya taifa la Afrika kusini. Maofisa zaidi wa polisi wametumwa …

Rais Zuma Ateta na JK Ikulu, Dk Bilal Amsindikiza

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya Desemba 22, 2014, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma. Mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, yalichukua kiasi cha saa moja na dakika 45 na yalihusu uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Rais Zuma ambaye aliwasili nchini usiku wa Desemba 21, 2014, …