RAIS wa Marekani Barrack Obama, amewapasha viongozi wa Afrika ambao wanaendelea kung’ang’ania madarakani hata baada ya Katiba kutowaruhusu kuendelea kuwania tena nyadhifa zao za urais. Katika hotuba ya kwanza ya Rais wa Marekani kwa muungano wa Afrika katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa, amesema kuwa Afrika haitapiga hatua iwapo viongozi wake watakataa kuondoka madarakani baada ya muda …
Rais Obama Kulitumia Jeshi Kupambana na Ebola
RAIS wa Marekani, Barack Obama amethibitisha wito wa kulitumia jeshi la nchi hiyo na wale wa akiba iwapo watahitajika kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Afrika magharibi. Rais Obama amesema wanajeshi hao wataongeza nguvu ya jeshi katika kutoa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo. Kundi la kwanza la wanajeshi hao linatarajiwa kupelekwa kusaidia ujenzi wa vituo 17 vya kutolea …
Rais Obama Kutumia Jeshi Kupambana na Ebola Afrika
RAIS wa Marekani, Barrack Obama ametangaza mpango wake wa kuwatuma wanajeshi 3,000 Afrika Magharibi kama njia mojawap ya kusaidia katika mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola. Rais Obama ametoa kauli hiyo huku akitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za dharura kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa Afrika ambao unaenea kwa kasi sana. Bwana Obama amesema …
Rais Obama Kupambana na Kundi la Wanamgambo Syria, Iraq
RAIS wa Marekani, Barack Obama ameahidi kuchukua hatua stahiki dhidi ya kikundi cha wanamgambo wa dola ya Kiislam huko Syria na Iraq. Katika hotuba yake kwa taifa hilo iliooneshwa kupitia televisheni ya taifa ameelezea mipango ya utekelezaji dhidi ya wanamgambo hao na kikundi chochote cha kigaidi kitakachoitishia Marekani hakitakua salama milele. Rais Obama pia amesema kwamba kikosi namba 475 watapelekwa …