RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa Mikoa, amewahamisha wengine sita na ameamua kuwa wengine watatu watapangiwa kazi nyingine. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mjini Dodoma, Novemba 5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa, Wakuu wapya wa Mikoa ni Bi. Halima Omari Dendego ambaye anakuwa Mkuu …
Rais Kikwete Aongoza Mamia Kumuaga Meja Jenerali Aidan Mfuse
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete leo, Novemba Mosi, 2014, ameongoza waombolezaji kuaga mwili wa Meja Jenerali Aidan Isidori Mfuse kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ya Lugalo, mjini Dar Es Salaam. Meja Jenerali Mfuse ambaye nambari yake ya usajili wa Jeshi ilikuwa P1624 alifariki dunia Oktoba 29, 2014, katika Hospitali …
JK Afagilia Kiwango cha Uwekezaji China
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema kuwa anafurahishwa na kiwango cha uwekezaji wa makampuni ya Jamhuri ya Watu wa China katika uchumi wa Tanzania ambao hadi mwishoni mwa mwaka jana ulikuwa umefikia miradi 522 yenye thamani ya dola za Marekani 2,490.21 milioni (dola bilioni 2.5). Rais Kikwete amesema kuwa kiwango hicho kinaufanya uwekezaji wa China katika …
Afrika ni Salama Licha ya Kuwepo Ugonjwa wa Ebola – Rais Kikwete
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ametoa changamoto kwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi za Afrika katika Jamhuri ya Watu wa China kuendelea kutangaza habari njema kuwa bado ni salama kutembelea Bara la Afrika pamoja na kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola ambao umeua maelfu ya watu hasa katika nchi tatu za Afrika Magharibi. Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa …
Rais Kikwete Aanza Ziara Rasmi ya Kikazi China
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete Oktoba 21, 2014, anaanza ziara rasmi ya siku sita katika Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping, ikiwa ni ziara yake ya pili nchini humo akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Baada ya China, Rais Kikwete atafanya ziara rasmi ya siku tatu nchini Vietnam kwa mwaliko wa …