ENDAPO ratiba ya madaktari wanaomtibu Rais Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Johns Hopkins nchini Marekani itakwenda kama ilivyopangwa kiongozi huyo atarejea nchini Tanzania, Novemba 29, 2014. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Taratibu za matibabu ya Rais Kikwete, zimekamilika Novemba 24, 2014. Taarifa hiyo imesema Rais Kikwete ataendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana …
Rais Kikwete Atuma Rambirambi Vifo vya Wanahabari
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara kuomboleza vifo vya Waandishi wa Habari, Innocent Munyuku wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd. na Baraka Karashani ambaye alikuwa Mwanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini. Mwandishi Mwandamizi, Innocent Munyuku alifariki akiwa …
Rais Kikwete Kuhamishiwa Hoteli Maalum kwa Uangalizi wa Madaktari
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anaendelea na matitabu yake nchini Marekani, Novemba 12, 2014, anatarajiwa kutoka wodini katika Hospitali ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye Hoteli Maalum ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari. Rais Kikwete amekuwa kwenye Hospitali ya Johns Hopkins tokea Jumamosi iliyopita wakati alipofanyikwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) na …
Rais Kikwete Afanyiwa Upasuaji Marekani…!
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Novemba 8, 2014, alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani. Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo. Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha …